Wednesday, May 27, 2020

UJE ROHO MTAKATIFU (Traditional)


Sauti zote zinavyoimbwa pamoja na nota. Click hapa
MANENO

  1. Uje Roho Mtakatifu Tuangaze toka Mbingu, Roho zetu kwa mwangao.
  2. Uje Baba wa maskini Uje mtoa wa vipaji, Uje mwanga wa mioyo.
  3. Ee Mfariji mwema sana Ee rafiki mwanana, Ewe Raha mustarehe.
  4. Kwenye kazi u-pumziko kwenye joto Burudisho, Umfutaji wa machozi.
  5. Ewe mwanga wenye heri uwajaze waamini, Neema yako mioyoni.
  6. Bila nguvu yako wewe mwanadamu hana kitu, Kwake yote yana kosa.
  7. Osha machafuko yetu panyeshee pakavu petu, Na kuponya majeraha .
  8. Ulegeze ukaidi pasha moto ubaridi, Nyoosha upotovu wetu.
  9. Wape waamini wako wenye tumaini kwako, Paji zako zote saba.
  10. Wape tuzo ya fadhila wape mwisho bila ila, Wape heri ya milele.
  11. Amina Aleluya Amina Aleluya, Amina Aleluya.


Friday, April 17, 2020

Bwana amefufuka

Bwana amefufuka kweli kweli Aleluya.
Utukufu na ukuu unayeye hata milele
Utukufu na ukuu unayeye
hata milele na milele

Umetungwa na Fr. G F Kayetta.

Pdf toka Swahilimusicnotes click hapa

Sikiliza sauti - click hapa

Sunday, April 12, 2020

MAGNIFICAT

Moyo, moyo wangu wamtukuza Bwana
Moyo moyo wangu wamtukuza Bwana
na roho yangu inaefurahi kwasababu ya Mungu Mwokozi wangu
na roho yangu inaefurahi kwasababu ya Mungu Mwokozi wangu

(Maneno ya Magnificat)
Muziki umetungwa na kuandikwa na Fr. Dr. Charles Nachinguru OFMCap (Jordan University) 16 Nov 2012
Pdf imetengenezwa na kupandishwa Swahili musicnotes na Emmanuel Mwita click hapa kuona
Clik hapa kusikiliza sauti na Muziki


Tuesday, March 24, 2020

KABILA LANGU

Kabila langu nimekutendea nini, au nimekusikitisha nini, nini?
Nijibu nijibu nijibu.

wa Ijumaa Kuu

Umetungwa na John Mgandu
Dar es salaam 11/03/1984

(Mungu ampokee kwenye furaha yake ya milele)

Pdf inapatikana Swahili Music notes Click hapa

Sikiliza sauti kwa headphones Click hapa.

Sunday, March 22, 2020

LAKINI HATA SASA ASEMA BWANA

Lakini hata sasa, asema Bwana.
Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote.

Mtunzi:- Aloyce Goden

Pdf inapatikana Swahili music notes click hapa

Sauti sikiliza Click hapa

Saturday, March 21, 2020

NALISEMA NITAYAKIRI

Nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana nawe
Bwana ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu

Mtunzi: B. Mapalala
O, bay DSM

Pdf inapatikana Swahilimusicnotes. Click hapa.

Mambo mengine yote click hapa

Sunday, March 15, 2020

Tuna Hazina hii

Tuna hazina hii katika vyombo vya udongo
Fr. Amedeus Kauki, OFMCap
Katika sikukuu yake ya kuzaliwa.

Pdf, Sauti mojamoja na wimbo wote click hapa