- Uje Roho Muumbaji / utazame Roho zetu / jaza neema za mbinguni / ndani ya viumbe vyako.
- Unaitwa mfariji / paji la Mwenyezi Mungu / Chanzo cha uzima, moto / pendo, mpako wa Rohoni.
- Mtoa wa vipaji saba / na kidole chake Mungu / Mwahidiwa naye Baba / na msemesha ndimi zetu.
- Tia nuru akilini / na upendo mioyoni / Tegemeza miili yetu / kwa imara yakudumu.
- Ufukuze mashetani / na amani tupe hima / Hivyo uwe kiongozi / tuepuke ovu lote.
- Umjulishe kwetu Baba / tukamjue pia Mwana / Tukakusadiki wewe / Roho na tokaye kwao.
- Atukuzwe Mungu Baba / na Mwanawe Mufufuka / Pia Roho Mtakatifu / kwa milele na milele/
Amina.
Tumia headphones usikie sauti
good choir i love the song
ReplyDeleteHow can I download audio
ReplyDelete