Wednesday, May 27, 2020

UJE ROHO MTAKATIFU (Traditional)


Sauti zote zinavyoimbwa pamoja na nota. Click hapa
MANENO

  1. Uje Roho Mtakatifu Tuangaze toka Mbingu, Roho zetu kwa mwangao.
  2. Uje Baba wa maskini Uje mtoa wa vipaji, Uje mwanga wa mioyo.
  3. Ee Mfariji mwema sana Ee rafiki mwanana, Ewe Raha mustarehe.
  4. Kwenye kazi u-pumziko kwenye joto Burudisho, Umfutaji wa machozi.
  5. Ewe mwanga wenye heri uwajaze waamini, Neema yako mioyoni.
  6. Bila nguvu yako wewe mwanadamu hana kitu, Kwake yote yana kosa.
  7. Osha machafuko yetu panyeshee pakavu petu, Na kuponya majeraha .
  8. Ulegeze ukaidi pasha moto ubaridi, Nyoosha upotovu wetu.
  9. Wape waamini wako wenye tumaini kwako, Paji zako zote saba.
  10. Wape tuzo ya fadhila wape mwisho bila ila, Wape heri ya milele.
  11. Amina Aleluya Amina Aleluya, Amina Aleluya.