KAR
Mwalimu wa Kwaya?
Nota zinasumbua?
Sasa unaweza
ku-download Karaoke Player iliyotengenezwa na Van Basco. (VanBasco's Karaoke
Player) ni ya bure kabisa. Itakuwezesha kufuatilia kwa urahisi sauti moja moja
na kuoanisha na maneno kwa urahisi kwa kufundisha. Sasa kwa nyimbo zile ambazo
nitatoa file lenye extension ya (.kar) unaweza kudownload file hilo na
kulifungua kwa kutumia player hiyo. Ni file dogo sana.
Kwa windows downloadhapa, click hapa, usikubali matangazo na mambo mengine
Ni program ndogo.
Inavyoonekana kwa
kifupi
Tazama vitufe chini, kila kitufe kinafungua window fulani na kitufe hicho hicho kinaifunga.
- Kilicho andikwa control nyuma yake kitakuwezesha kubadili , mwendo (tempo) funguo (key) na ukubwa wa sauti (volume)
- Kilicho andikwa Karaoke nyuma yake kitakuwezesha kufuatilia maneno yaliyo kwenye muziki
- Kilicho andikwa output nyuma yake kitakuwezesha kuchagua sauti ya kusikiliza. Vya rangi nyekundu vinanyamazisha sauti fulani (mute) na vya blue vina chagua sauti fulani isikike peke yake. (solo)
- Kilichoa andikwa piano nyuma yake kitakuonyesha mmm uchezaji.
RUDI MWANZO Click hapa
No comments:
Post a Comment