Thursday, May 3, 2018

Uje Roho Muumbaji

By Dr. Mbilinyi (1990 DSM)

  • Uje Roho Muumbaji / utazame Roho zetu / jaza neema za mbinguni / ndani ya viumbe vyako.
  • Unaitwa mfariji / paji la Mwenyezi Mungu / Chanzo cha uzima, moto / pendo, mpako wa Rohoni.
  • Mtoa wa vipaji saba / na kidole chake Mungu / Mwahidiwa naye Baba / na msemesha ndimi zetu.
  • Tia nuru akilini / na upendo mioyoni / Tegemeza miili yetu / kwa imara yakudumu.
  • Ufukuze mashetani / na amani tupe hima / Hivyo uwe kiongozi / tuepuke ovu lote.
  • Umjulishe kwetu Baba / tukamjue pia Mwana / Tukakusadiki wewe / Roho na tokaye kwao.
  • Atukuzwe Mungu Baba / na Mwanawe Mufufuka / Pia Roho Mtakatifu / kwa milele na milele/

Amina.


Tumia headphones usikie sauti

1 comment: